Nabi Afunguka Sababu za Kumchagua Mayele-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Nabi Afunguka Sababu za Kumchagua Mayele-Michezoni leo

KOCHA wa Yanga, Nasreedin Nabi amesema kuwa anachagua kuanza na Fiston Mayele kwenye kila mchezo wa ligi kuu kwa kuwa nyota huyo anapendwa na mashabiki na kuifanya kazi yake vema.

 

Nabi alifunguka kuwa amekuwa akisikia maoni ya watu ya kwanini hampi nafasi ya kucheza Heritier Makambo lakini ukweli ni kwamba hawezi kumweka nje mchezaji ambaye amekuwa akifanya vizuri kwenye kila mchezo.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Nabi alisema Makambo ni mchezaji mzuri na amekuwa akionyesha bidii kwenye uwanja wa mazoezi, ila kuna vitu bado hajavipata ambavyo Mayele anafanya na anahisi kwa kuwa alikosa muda wa kucheza akiwa Horoya.

 

“Mashabiki wanampenda Mayele na anafanya vizuri sana akiwa uwanjani, mimi kama kocha siwezi kumweka nje mchezaji ambaye anafaya kazi nzuri uwanjani. “Nasikia mashabiki baadhi wakihoji juu ya kwanini Makambo hachezi, siyo mchezaji mbaya anaonyesha jitihada kubwa sana kwenye uwanja wa mazoezi.

 

“Ila kuna sehemu bado kidogo anatakiwa aongeze kasi nafikiri kwa sababu ya kukosa muda wa kucheza kule Horoya. Huwa nazungumza naye mara kwa mara na anaelewa,” alisema.

The post Nabi Afunguka Sababu za Kumchagua Mayele appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz