Mwamuzi Simba vs Yanga Awekwa Mtu Kati-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mwamuzi Simba vs Yanga Awekwa Mtu Kati-Michezoni leo

ZIKIWA zimebaki takribani siku nne kabla ya mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Yanga, mwamuzi wa kati atakayechezesha mechi hiyo tayari amejulikana baada ya kufanyika kikao kizito.

 

Jumamosi hii, Simba itakuwa mwenyeji wa Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Mpaka sasa, majina ya waamuzi watatu yameonekana kupenya kwenye kamati ya waamuzi na mmoja kupewa jukumu la kuamua mchezo huo.

 

Taarifa kutoka chanzo cha kuaminika, zimeliambia Spoti Xtra kuwa, kinachowafanya waweze kuchagua waamuzi ni namna ambavyo wameweza kusimamia mashindano husika na kufuata sheria 17 za soka.

 

Mtoa taarifa huyo alisema kwamba, hivi karibuni kamati ilikuwa na kikao kizito kumchagua mwamuzi huyo na anatarajiwa kutangazwa rasmi kati ya leo Jumanne au kesho Jumatano.

Waamuzi hao watatu wanaotajwa huenda mmoja akapewa nafasi hiyo ni Herry Sasii, Ahmed Arajiga na Ramadhan Kayoko.

 

Kwenye mchakato huo kuna majina ya waamuzi wanne ambayo yamekuwa ni pasua kichwa kutokana na waamuzi kulalamikiwa kutokana na maamuzi yao kuwa na utata ambao ni Emmanuel Mwandembwa, Abel William, Hance Mabena na Martin Saanya.

 

Pia kuna uwezekano wa mwamuzi huyo akawa mgeni kuchezesha mechi hiyo ambapo wanaotajwa ni Joseph Akamba, Raphael Ikambi na Nassoro Mwichui.Mjumbe wa Kamati ya Waamuzi, Sud Abdi, aliliambia Spoti Xtra kuwa: “Siku zimebaki chache kuelekea huo mchezo, hivyo kama kamati tunaendelea na mchakato, taarifa kwa umma itatolewa kati ya kesho (leo) au kesho kutwa (Jumatano).

STORI NA LUNYAMADZO MLYUKA NA LEEN ESSAU | SP[OTI XTRA

The post Mwamuzi Simba vs Yanga Awekwa Mtu Kati appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz