Morrison Anaitaka Azam FC-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Morrison Anaitaka Azam FC-Michezoni leo

UNAAMBIWA pamoja na Kiungo Mshambuliaji wa Simba raia wa Ghana, Bernard Morrison kukosekana kwa muda ndani ya timu hiyo akiwa ameenda kwao, lakini bado ametuma ujumbe kwa kocha wa timu hiyo, Pablo Franco akiomba awepo kwenye kikosi kitakachocheza dhidi ya Azam FC, wikiendi hii.


Morrison alitarajiwa kutua nchini
mapema jana Jumatano tayari kwa kuungana na wenzake kujiandaa na mchezo huo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Chanzo chetu kutoka Simba, kimeliambia Spoti Xtra kuwa: “Kiukweli Morrison ana mapungufu yake ila linapokuja suala la kupigania namba, hajawahi kurudi nyuma.


“Licha ya kuwa safarini kwa
muda, bado amekuwa akiwasiliana na kocha wetu, akimuomba sana hata kama ataingia nchini akiwa amechelewa basi ampatie nafasi ya kucheza dhidi ya Azam FC.


“Morrison ametua
jana tayari kwa kuungana na wenzake, ila pamoja na hilo anashauku kubwa sana ya kuonesha jambo katika mchezo huo.”

STORI: MUSA MATEJA, DAR

The post Morrison Anaitaka Azam FC appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz