Mbeya Kwanza Wakubali Kuwapa Yanga Straika-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mbeya Kwanza Wakubali Kuwapa Yanga Straika-Michezoni leo

WAKATI kukiwepo na tetesi za Yanga kumuhitaji straika Chrispin Ngushi, mabosi wa straika huyo Mbeya Kwanza wameibuka na kubainisha kuwa wapo tayari kumuachia nyota huyo kutua Jangwani.


Ngushi amekuwa na msimu
mzuri hadi sasa akiwa na Mbeya Kwanza ambapo ameweka kambani mabao matatu na asisti moja.


Akizungumza na
Championi Jumamosi, Mwenyekiti wa Mbeya Kwanza, Mohammed Mashango alisema kuwa endapo Yanga watakuwa tayari kwa ajili ya mazungumzo basi wao kama timu watamuachia mchezaji huyo.


“Hadi sasa bado hatujapata
ofa yoyote kutoka kwa Yanga lakini tumekua tukisikia kuwa wanamuhitaji lakini bado hawajafika kwetu kama wakija tukafanya mazungumzo na tukafikia makubaliano mazuri basi kila kitu kitakuwa wazi.


“Sisi kama timu tupo tayari
kumuachia Chrispin kwenda Yanga kwani lengo letu ni kuona vijana wetu wanakuza vipaji, kwa hiyo hatutakuwa na pingamizi kwenye jambo hilo,” alisema Mashango.

HAWA ABOUBAKHARI, Dar es Salaam

The post Mbeya Kwanza Wakubali Kuwapa Yanga Straika appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz