Mashine Mpya Yaahidi Mabao Yanga-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mashine Mpya Yaahidi Mabao Yanga-Michezoni leo

JEMBE jipya la Yanga, Chico Ushindi amefunguka kuhitaji kutengeneza nafasi nyingi za mabao ambazo pindi atakapoanza kuitumikia rasmi Yanga ambazo zitawafanya mastraika wa timu hiyo wakiongozwa na Fiston Mayele na Heritier Makambo kufunga mabao ya kutosha.


Ushindi ambaye anamudu kucheza
winga zote ni usajili mpya kwa Yanga ambaye amesajiliwa kwa mkopo
akitokea katika Klabu ya TP Mazembe
ya nchini DR Congo.


Akizungumza na Championi
Jumamosi, Ushindi aliweka wazi kuhitaji kutengeneza nafasi nyingi za kufunga kwa washambuliaji wa timu hiyo pindi atakapoanza kuitumikia rasmi Yanga katika michezo mbalimbali ambayo wanashiriki msimu huu.


“Yanga tayari nimeshaona jinsi
ambavyo wanacheza, ni timu ambayo inatumia sana wachezaji wa pembeni katika kutengeneza nafasi za kufunga. Mimi pia nacheza huko hivyo naona nafasi ya kutengeneza zaidi nafasi za
kufunga kwa washambuliaji wa kati.

 

“Kusajiliwa na kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza mara kwa mara ni jambo jingine, hivyo ngoja tuone itakuwaje lakini nahitaji kucheza ili kuweza kuisaidia Yanga kufanya vizuri pamoja na kubeba ubingwa wa ligi kuu,” alisema winga huyo.

STORI: MARCO MZUMBE, Dar es Salaam

The post Mashine Mpya Yaahidi Mabao Yanga appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz