Kocha Simba Aionya Yanga-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Kocha Simba Aionya Yanga-Michezoni leo

WAKATI Simba ikiwa Zambia katika michuano ya Kimataifa, kocha msaidizi wa timu hiyo, Thierry Hitimana raia wa Rwanda amefichua kuwa kuwa bize katika michuano ya kimataifa kusiwafanye wapinzani wao Yanga wakajisahau kuelekea kwenye mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Bara kwa kuwa malengo yao ni kushinda mchezo huo.

 

Hitimana ametoa kauli hiyo ikiwa jana Jumapili Simba ilicheza mchezo wa pili wa hatua ya mtoano kwenye Kombe la Shirikisho Afrika kabla ya kurejea nchini kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga ambao unatarajia kupigwa Desemba 11, mwaka huu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Hitimana alisema kuwa uwepo wao katika michuano ya kimataifa wapinzani wao katika Ligi Kuu Bara wasitumie kama kigezo cha wao kuwa wepesi kwa kushindwa kupata matokeo mazuri kwenye mchezo ujao kwa kuwa wamejipanga vizuri.

 

“Kitu kikubwa nadhani kila mtu anaelewa ukubwa na presha ya mchezo wa dabi inavyokuwa kwa sababu kila upande umekuwa ukitafuta matokeo ili kuwa katika nafasi nzuri kwenye ushindani wa kuelekea mwisho wa msimu.

 

 

“Unajua Simba tunashiriki michuano ya kimataifa lakini haiwezi kuwa sababu ya kushindwa kufanya maandalizi ya mchezo huo popote ambapo tutakuwa hivyo wasifikirie kama tutakuwa wepesi,” alisema Hitimana.

The post Kocha Simba Aionya Yanga appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz