KMC hawana bahati na mechi zao za vigogo-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

KMC hawana bahati na mechi zao za vigogo-Michezoni leo

KLABU ya KMC kwa msimu wa 2021/22 kwenye mechi zao mbili za vigogo ndani ya ligi hawajawa na bahati ya kusepa na pointi tatu zaidi walikuwa wakiambulia maumivu ya kunyooshwa.

Ikumbukwe kwamba KMC makazi yao yapo Dar lakini kwa mechi zilizokuwa zikiwakutanisha dhidi Yanga na Simba walikuwa wakizipeleka nje ya Dar.

Ilikuwa ni ile dhidi ya Yanga iliyochezwa Uwanja wa Majimaji, Songea, Oktoba 19, ubao ulisoma KMC 0-2 Yanga na ile ya pili ilikuwa dhidi ya Simba Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora Desemba 24 na ubao ulisoma KMC 1-4 Simba.

Katika mechi mbili ambazo ni dakika 180 walizocheza nje ya Dar, KMC imeyeyusha pointi sita mazima huku ikifungwa jumla ya mabao saba na ni bao moja safu yake ya ushambuliaji ilifunga.

Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala aliliambia Championi Jumatatu kuwa sababu kubwa ya kupeleka mechi nje ya Dar ni kuweza kuwafikia mashabiki wao.

“Tuna mashabiki wengi ambao wanaitambua KMC lakini wanahitaji kuiona, kuhusu matokeo ni suala ambalo linatokea na tunaamini kwamba benchi la ufundi litafanyia kazi upungufu,” alisema.

LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam

The post KMC hawana bahati na mechi zao za vigogo appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz