Kisubi: Utu Wangu ni Bora Kuliko Kitu-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Kisubi: Utu Wangu ni Bora Kuliko Kitu-Michezoni leo

 

ALIYEKUWA kipa wa Simba Sc, Jeremiah Kisubi amewashukuru uongozi na mashabiki wa klabu hiyo kwa kipindi alichohudumu huku akisema kuwa, ameamua kufanya maamuzi ya kuondoka msimbazi ili kulinda utu wake.

 

Kisubi ambaye ametimkia Mtibwa Sugar kwa mkopo amesema; “Sijazoea kuishi chini ya kivuli mara zote naamini ninachokifanya. Na Mungu atailinda heshima yangu iliyoshushwa kilazima.

 

“Nawapenda napenda kila kitu kutoka kwenu naheshimu ukubwa wa klabu nawatakia kila kilicho chema tutaishi milele kwa kuwa mimi bado ni sehemu yenu. Ila utu wangu ni bora kuliko kitu,” amesema Kisubi.

 

Kisubi ambaye alijiunga na Simba katika dirisha kubwa la usajili wa msimu huu mnamo Agosti 18, mwaka huu akitokea Tanzania Prisons ya Mbeya amekosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Simba jambo ambalo limepelekea kuandika barua kwa uongozi wa timu hiyo kuomba kutolewa kwa mkopo kwenda.

The post Kisubi: Utu Wangu ni Bora Kuliko Kitu appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz