Jeraha Lamaliza Pambano la Kidunda-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Jeraha Lamaliza Pambano la Kidunda-Michezoni leo

JERAHA alilolipata bondia Selemani Kidunda katika raundi ya tatu limesababisha kumalizwa bila mshindi (kwa sare) katika pambano la kusaka ubingwa wa IBF dhidi ya bondia kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Tshimanga Katompa usiku wa kuamkia leo.

Kidunda alichanika juu ya paji lake la uso baada ya kugongwa na kichwa cha Katompa jambo lililomsababishia kushindwa kuendelea na pambano hilo kutokana na kuvuja damu nyingi kwasababu ya jeraha kuwa kubwa.

Kwamujibu wa msimamizi wa mkanda huo ni kuwa bondia Selemani Kidunda angeweza kupewa ushindi endapo pambano hilo lingefika raundi ya nne kwani jerahi alilolipata lilitokana na kuchezewa mchezo usio wa kiungwana kwa makusudi na mpinzani wake aliyetumia kichwa kumjeruhi lakini sheria za IBF zinawalazimu kutoa matokeo ya sare kwasababu tu tatizo hilo limejitokeza katika raundi ya tatu.

Hata hivyo upande wa Bondia Katompa amelalamikia uamuzi wa kumaliza pambano hilo akiamini mpinzani wake angeweza kuendelea na mchezo huo baada ya kupatiwa matibabu.

Bondia Kidunda yeye amemlaumu Katompa kwa kumsababishia jeraha hilo kwa makusudi na kusema kuwa amemchafulia rekodi yake kwani hajawahi kutoka sare katika mapambano yake. Pambano hilo lilikuwa la raundi kumi.

The post Jeraha Lamaliza Pambano la Kidunda appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz