Jembe la Mazembe Mali ya Yanga-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Jembe la Mazembe Mali ya Yanga-Michezoni leo

HATIMAYE uongozi wa Klabu ya TP Mazembe, umethibitisha kumalizana na Yanga juu ya usajili wa mchezaji Chico Ushindi Wakubenza, huku ukiweka wazi tarehe ya mchezaji huyo kutua rasmi kujiunga na mabingwa hao wa kihistoria hapa nchini.


Hivi karibuni Ofisa Habari
wa Yanga, Hassan Bumbuli,  aliweka wazi kuwa klabu hiyo itafanya usajili wa baadhi ya wachezaji kutokana na timu hiyo kukumbwa na majeruhi ya wachezaji wao muhimu akiwemo Yacouba Songne, Fiston Mayele, Kibwana Shomari na Yusuph Athuman.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Mratibu wa Mashindano wa TP Mazembe anayefahamika kwa jina la Jean Kazadi, alisema taratibu zote za usajili wa Chico Ushindi kwenda Yanga zimeshakamilika, hivyo kilichobaki ni mchezaji huyo kumalizia baadhi ya michezo mpaka Desemba 28, mwaka huu, kisha kuanza safari ya kuja Dar kujiunga na Yanga.

 

“Chiko Ushindi tayari uongozi wa Mazembe na Yanga tumekamilisha mazungumzo ya usajili,mchezaji huyo kwa sasa anasubiri kukamilisha michezo miwili nje ya Lubumbashi tuliyonayo, kisha tarehe 28 mwezi huu atarejea Lubumbashi kwa ajili ya kuanza taratibu za safari yake ya kuja huko Tanzania kujiunga na Yanga.


“Hivi ninavyokuambia
Ushindi ni mali ya Yanga na amejiunga na timu hiyo kwa mkopo wa muda mrefu wenye vipengele vya kubaki Yanga moja kwa moja pindi watakapoona anawafaa au kumuuza, kisha pesa tukagawana, sisi na wao Yanga.


“Kusema ukweli Yanga
wamepata mchezaji mzuri sana ambaye atakuja kuwasaidia kwa kuwa ni moja kati ya wachezaji ambao nikitazama katika kikosi chao hata Jesus Moloko na yule Tuisila Kisinda hawawezi kumfikia kwa ubora, Yanga wenyewe wataona ubora wake,” alisema kiongozi huyo.

MARCO MZUMBE, Dar es Salaam

The post Jembe la Mazembe Mali ya Yanga appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz