Hitimana Ataja Sababu za Kuondoka Simba-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Hitimana Ataja Sababu za Kuondoka Simba-Michezoni leo

BAADA ya Klabu ya Simba kutangaza kufikia muafaka wa pande mbili kuvunja mkataba wa kocha msaidizi wa timu hiyo, Hitimana Thierry, mwenyewe ameibuka na kufunguka sababu kubwa ya kuondoka kikosini hapo.


Juzi Jumanne, Simba
ilitoa taarifa hiyo ikiwa ni takribani miezi mitatu imepita tangu Hitimana raia wa Burundi kujiunga na Simba Septemba, mwaka huu.


Akizungumza na Spoti
Xtra, Hitimana alisema sababu kubwa ya yeye kuondoka Simba ni baada ya waajiri wake hao kushindwa kutimiza baadhi ya makubaliano waliyoingia wakati anasaini mkataba.


“Kumekuwa na taarifa
nyingi zinazohusishwa na uamuzi wa mimi kuondoka Simba, lakini ukweli ni kwamba nimeachana na Simba kutokana na mambo mbalimbali.


“Kubwa zaidi ni
kutotimiziwa yale ambayo yalikuwepo kwenye makubaliano wakati ninaingia nao mkataba, hivyo nikaona ni jambo bora kufikia muafaka wa pamoja tuachane salama.”

STORI: IBRAHIM MUSSA NA JOEL THOMAS, Dar

The post Hitimana Ataja Sababu za Kuondoka Simba appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz