GSM Yawafanyia Kufuru Mastaa Yanga-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

GSM Yawafanyia Kufuru Mastaa Yanga-Michezoni leo

WADHAMINI wa Yanga ambao ni GSM, wamewafanyia kufuru mastaa wa timu hiyo kwa kuwapatia vocha yenye thamani ya Sh milioni moja kila mchezaji iliyotumika kufanya shopping katika maduka yote ya GSM Group Limited.


Hiyo ikiwa ni siku chache tangu
Yanga itoke kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Biashara United katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.


Mmoja wa wachezaji wa
Yanga, ameliambia Spoti Xtra kuwa: “Katika kusherehekea Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya, wachezaji wote tumepewa vocha yenye thamani ya shilingi milioni moja itakayotumika kufanya shopping katika maduka ya GSM.


“Wachezaji wote jana (juzi)
tulifika Msasani Mall kwa ajili ya kuchukua mahitaji ikiwemo nguo, viatu na vitu vingine
vyenye thamani hiyo.”


Nahodha wa Yanga, Bakari
Mwamnyeto, alitumia ukurasa wake wa Instagram kuandika ujumbe wa kumshukuru bosi wa GSM ulisomeka hivi: “Shukran Boss GSM kwa zawadi ya leo (jana). Tunashukuru kwa ulichotupa dukani na sisi tutakupa uwanjani, kila hatua dua. Mungu wetu sote.”

STORI: WILBERT MOLANDI NA MUSA MATEJA, Dar es Salaam

The post GSM Yawafanyia Kufuru Mastaa Yanga appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz