TIMU ya Chelsea imekamilisha mechi zake za Kundi H kwa sare ya ugenini ya 3-3 dhidi ya Zenit St Petersburg Uwanja wa Saint-Petersburg Stadium Jijini St. Petersburg.
Mabao ya Chelsea yamefungwa na Timo Werner mawili, dakika ya pili na 85 na Romelu Lukaku dakika ya 62, wakati ya Zenit yamefungwa na Claudinho dakika ya 38, Sardar Azmoun dakika ya 41 na Magomed Ozdoyev dakika ya mwisho kabisa.
Pamoja na hayo, Chelsea imetinga 16 Bora baada ya kumaliza nafasi ya pili Kundi H kwa pointi zake 13, ikizidiwa mbili na Juventus walioongoza, wakati Zenit imemaliza na pointi tano na Malmo moja.
No comments:
Post a Comment