Bosi Yanga: Simba Haitupi Presha-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Bosi Yanga: Simba Haitupi Presha-Michezoni leo

SENZO Mbatha, Mtendaji Mkuu wa Yanga SC amebainisha kwamba hawana presha na watani zao wa jadi, Simba kuelekea kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Desemba 11, mwaka huu.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Mbatha alisema kuwa wanatambua kuhusu mchezo huo kwa kuwa upo kwenye ratiba, hivyo watafanya maandalizi mazuri ili kupata ushindi.


“Ipo wazi kwa muda mrefu
kwamba lazima tutakutana na Simba kwenye mechi ya ligi, hivyo hakuna presha kuelekea mchezo huo, kila kitu kinakwenda sawa na maandalizi yake ni kama ilivyo kwenye michezo
mingine.


“Mwendo ambao
tunakwenda nao ninaamini kwamba mashabiki wanaona, hivyo hakuna haja ya kuwa na mashaka
juu ya uwezo wa wachezaji
wetu ambao wapo kwani kila mmoja anafanya kazi kwa umakini katika
kutimiza majukumu yake,”
alisema Mbatha.

STORI: LUNYAMADZO MLYUKA, DAR

The post Bosi Yanga: Simba Haitupi Presha appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz