Beki wa Arsenal Gabriel Apambana na Majambazi Gereji Kwake-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Beki wa Arsenal Gabriel Apambana na Majambazi Gereji Kwake-Michezoni leo

Nyota wa Klabu ya Arsenal, Gabriel Magalhaes amekabiliana na wezi waliokuwa wameficha nyuso zao na kujihami kwa silaha ikiwemo marungu ambao walivamia katika gereji ya mwanasoka huyo na kujaribu kuiba gari lake.

 

Wezi hao ambao walikuwa watatu walimfuata Gabriel kimya kimya mpaka nyumbani kwake eneo la Barnet London Agosti 20, mwaka huu na kumtaka awapatie funguo zake za gari lake.

 

Kanda ya video ya tukio hilo ambayo imeonekana juzi inamuonesha Gabriel akijaribu kukabiliana na mtu aliyebeba rungu la mchezo wa baseball ambaye baadaye alijulikana kama Abdi Muse.

 

Muse mwenye umri wa miaka 26 alihukumiwa kifungo cha miaka 5 jela kwa makosa ya wizi wa kutumia nguvu katika mahakama ya Harrow Crown mnamo tarehe 17 Novemba.

 

Baada ya kuzidiwa nguvu mwizi huyo alitoroka na funguo za gari la Gabriel lakini akaliwacha gari hilo nyuma katika gereji. Baadaye jamaa huyo alikamatwa na maafisa wa polisi na kushtakiwa na wizi wa mabavu na kumiliki silaha hatari.

The post Beki wa Arsenal Gabriel Apambana na Majambazi Gereji Kwake appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz