Barbara: Tunahitaji Pointi Tatu za Yanga-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Barbara: Tunahitaji Pointi Tatu za Yanga-Michezoni leo

MTENDAJI Mkuu wa Klabu ya Simba Barbara Gonzalez amesema kuwa hawataki kurudia makosa waliyofanya kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga na watahitaji alama tatu Desemba 11.

 

Barbara alifunguka kuwa wamefanya kila kitu ili kuhakikisha timu inapata alama tatu mbele Yanga kwa sababu hiyo ni moja ya njia ya kutetea ubingwa wao wa ligi kuu pamoja na kufanya vizuri zaidi msimu huu.

 

Barbara alisema baada ya kumalizana na Red Arrows ambao walikuwa wanacheza nao jana kwenye Uwanja wa Heroes Lusaka Zambia akili na mipango yao inahamia kwenye dabi.

 

“Baada ya kumaliza majukumu yetu na Red Arrows tutahamia kwenye mipango ya mchezo wetu na Yanga Desemba 11, tunahitaji kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi.

 

“Ili tufike hapo inatakiwa lazima tushinde mechi ya dabi, hakuna jambo lingine ambalo Wanasimba watakuwa wanahitaji zaidi ya alama tatu kwenye mchezo huo,” alisema.

 

Kama Simba walifanikiwa kushinda mchezo wao wa jana dhidi ya Red Arrows watakuwa wamekata tiketi ya kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

The post Barbara: Tunahitaji Pointi Tatu za Yanga appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz