Barbara: Simba Tupo Imara, Wachezaji Wanajituma-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Barbara: Simba Tupo Imara, Wachezaji Wanajituma-Michezoni leo

 

MTENDAJI Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez ameweka wazi kuwa Simba ipo imara na hesabu kubwa
ni kutimiza malengo
waliyojiwekea kutokana na wachezaji walionao kujituma.


Kwa sasa Simba
inapambana kuweza kutetea taji lake ililotwaa msimu uliopita wakivutana kwa kasi na vinara wa ligi ambaoni Yanga wenye pointi 23 huku Simba wakiwa nafasi ya pili na pointi 18 kabla ya mchezo wa jana dhidi ya KMC.


Akizungumza na
Championi Jumamosi, Barbara alisema kuwa wanazidi kufanya mambo
mazuri kwa ajili ya timu.


“Tupo imara kwa namna
ambavyo tunafanya hivyo mashabiki wasiwe na mashaka na sisi katika yale ambayo tunafanya, wachezaji wanajituma katika kutimiza majukumu yao.


“Imani yetu ni kwamba
tutafanya vizuri kwenye ligi na kwenye Kombe la Shirikisho kwani haya nayo ni mashindano makubwa kimataifa kwa kuwa tupo kuiwakilisha nchi kimataifa, mashabiki wazidi kutuombea,” alisema Barbara.

The post Barbara: Simba Tupo Imara, Wachezaji Wanajituma appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz