Azam, Kagera Sugar Kazi Ipo-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Azam, Kagera Sugar Kazi Ipo-Michezoni leo

WAKATI Desemba 9, mwaka huu Azam ikitarajiwa kuwa mwenyeji wa Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar, kila upande umepania kuibuka na ushindi.

 

Mshambuliaji wa Azam, Idriss Mbombo, amesema amejipanga kuwamaliza Kagera Sugar kwenye mchezo huo ili kuipa timu yake alama tatu.


Akizungumza na Spoti Xtra,
Mbombo mwenye mabao mawili, amesema: “Nina hamu ya kuwafunga Kagera na kuipa
alama tatu timu yangu.
“Nina imani mpaka ligi inamalizika ninaweza kuwa mfungaji bora maana timu yangu inanipa sapoti kubwa.”

 

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Francis Baraza, ameweka wazi kuwa: “Tumetoka kupoteza
mchezo ugenini dhidi ya Ruvu
Shooting, kwa sasa tumejaribu kufanya mabadiliko makubwa na thabiti yenye ubora wa hali ya juu, tunaamini mchezo ujao dhidi ya Azam tutafanya vizuri.


“Kwa upande wa wachezaji,
kikosi kipo tayari isipokuwa tuna majeruhi wawili ambao hawataweza kushiriki mchezo
huo, waliobaki wote wapo
vizuri kiafya, niwatoe wasiwasi mashabiki zetu tumejiandaa vya kutosha kupata ushindi.”

STORI NA CAREEN OSCAR NA ELIZABETH MISANA (DSJ)

The post Azam, Kagera Sugar Kazi Ipo appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz