Atletico Wakichafua, Watinga 16 Bora Kibabe-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Atletico Wakichafua, Watinga 16 Bora Kibabe-Michezoni leo

WAGUMU wa Atletico Madrid wameweza kufuzu hatua ya 16 Bora ligi ya mabingwa barani Ulaya baada ya kuwafunga FC Porto 3-1 nyumbani.

 

Mchezo huo wa vuta nikuvute ulishuhudiwa jumla ya kadi nyekundu tatu zikitoka huku wachezaji wa FC Porto Wendell na Agustin Marchesin wakioneshwa kadi hizo dakika za 70 na 75 huku Yannick Carrasco wa Atletico Madrid akitangulia kulambwa kadi nyekundu dakika ya 67.

 

Hata hivyo mabao ya Antoine Griezmann na yale ya dakika za nyongeza ya Angel Corea na Rodrigo De Paul yakawapa tiketi Atletico Madrid kufuzu kwa hatua inayofuata ya ligi ya mabingwa Ulaya huku Porto wakiporomka hadi kwenye michuano ya Ligi ya Uropa.

 

Liverpool, Atletico, Real Madrid, Ajax, Sporting CP, Inter zafuzu 16 bora Klabu Bingwa Ulaya.

Matokeo 

FC Porto 1-3 A. Madrid
AC Milan 1-2 Liverpool
Ajax 4-2 Sporting CP
Dortmund 5-0 Besiktas
Real Madrid 2-0 Inter
Shaktar 1-1 FC Sheriff.

The post Atletico Wakichafua, Watinga 16 Bora Kibabe appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz