Arsenal Yatinga Nusu Fainali Carabao Cup-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Arsenal Yatinga Nusu Fainali Carabao Cup-Michezoni leo

Washika mitutu wa London, Arsenal wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup baada ya ushindi wa 5-1 dhidi ya Sunderland usiku wa jana Uwanja wa Emirates Jijini London.

Shujaa wa Arsenal jana alikuwa ni mshambuliaji Eddie Nketiah aliyefunga mabao matatu peke yake dakika za 17, 49 na 58, wakati mabao mengine yamefungwa na Nicolas Pepe dakika ya 27 na kinda wa umri wa miaka 18 aliyekuwa anacheza kwa mara ya kwanza kikosi cha kwanza, Charlie Patino dakika ya 90+1.

Mechi nyingine tatu za hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya Carabao Cup zitapigwa leo.

The post Arsenal Yatinga Nusu Fainali Carabao Cup appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz