Zaha Akimbia Timu ya Taifa Ivory Coast-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Zaha Akimbia Timu ya Taifa Ivory Coast-Michezoni leo

STAA wa Crystal Palace, Wilfried Zaha ameomba asijumuishwe  kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Ivory Coast kinachojiandaa na michezo ya kufuzu kombe la Dunia dhidi ya Cameroon na Msumbiji.

 

Kocha wa Ivory Coast Patrice Beaumelle amesema Zaha huwa anaumwa kila anaporudi kutoka kwenye majukumu ya taifa hilo, na anaendelea kutafakari juu hatma yake kwenye soka la Kimataifa.

 

“Ameomba tusimjumuishe kwa sababu anarudi nyumbani akiwa anaumwa kila anapotoka kwenye majukumu ya timu ya Taifa” amesema kocha Beamelle.

 

Zaha ambaye alibadili uraia mwaka 2017, baada ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha England, ameichezea Ivory Coast mechi 21 na kufunga magoli 5.

The post Zaha Akimbia Timu ya Taifa Ivory Coast appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz