Yanga Yatangaza Hali ya Hatari-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Yanga Yatangaza Hali ya Hatari-Michezoni leo

UONGOZI wa klabu ya Yanga umetamba kuwa moto walioanza nao kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu hauzimiki, bali wataendelea kukusanya pointi tatu katika kila mchezo ulio mbele yao ili kutimiza jambo lao la kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

 

Yanga wameanza vizuri msimu huu ambapo mpaka sasa kwenye Ligi Kuu ndio vinara wa msimamo, wakiwa wamejikusanyia pointi 15 baada ya kuibuka na ushindi katika michezo yao mitano waliyocheza.

Mchezo ujao wa Yanga ni wa ugenini dhidi ya Namungo utakaopigwa Novemba 20, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi.

 

Akizungumza na Global Publishers, Ofisa habari wa klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli alisema: “Kwetu sisi nguvu kubwa tumewekeza katika timu yetu kuhakikisha tunafanya vizuri katika kila mchezo ulio mbele yetu ili kufanikisha dhumuni la kushinda ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.

 

“Tunajua ligi ya msimu huu ni ngumu, lakini tunajivunia ubora wa kikosi tulichonacho ambao kwa kiasi kikubwa tuna uhakika kinaweza kutimiza malengo tuliyojiwekea.”

JOEL THOMAS, Dar es Salaam

The post Yanga Yatangaza Hali ya Hatari appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz