Yanga Yaiandalia Dozi Mbeya Kwanza-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Yanga Yaiandalia Dozi Mbeya Kwanza-Michezoni leo

LEO Jumanne, Mbeya Kwanza watawakaribisha Yanga ambao ni vinara kwenye Ligi Kuu Bara, katika mchezo wa ligi hiyo utakaochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.


Yanga ambayo imetua
jijini Mbeya tangu juzi Jumapili, imepania kufanya kweli na kushinda mchezo huo, huku wenyeji wao nao wakisema hawatakubali kufungwa.


Kocha wa
Mbeya Kwanza, Harerimana Haruna, aliliambia Spoti Xtra kuwa: “Mchezo siyo rahisi, kwa sababu tunakwenda kukutana na timu bora msimu huu, tumejiandaa kushindana na kutafuta ushindi.


“Yanga wanacheza vizuri na kila
mtu anaona, mwisho wa siku huu ni mpira na matokeo hupatikana baada
ya dakika 90.

 

Kwa uwezo wa Mungu tunaenda kufanya vizuri.”Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM na Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Injinia Hersi Said, alisema: “Mbeya ni kama nyumbani, awamu hii siyo kama awamu nyingine zilizopita, tumekuja kutafuta alama tatu na siyo jambo lingine.

Najua haitakuwa rahisi kwetu, ila lazima tushinde.”

STORI NA ISSA LIPONDA | CHAMPIONI

The post Yanga Yaiandalia Dozi Mbeya Kwanza appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz