Yanga Warejea Bongo Kutoka Zanzibar-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Yanga Warejea Bongo Kutoka Zanzibar-Michezoni leo

BAADA ya kukamilisha kambi ya muda Zanzibar kwa ajili ye kujiweka sawa kwa mechi za Ligi Kuu Bara leo Novemba 13 kikosi cha Yanga kimerejea Dar.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ilikuwa Zanzibar na imecheza mechi mbili za kirafiki.

Mchezo wa kwanza ulikuwa dhidi ya Mlandege FC na ule wa pili ulikuwa dhidi ya KMKM FC, Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Mechi zote mbili Yanga iliibuka na ushindi ambapo ule wa kwanza dhidi ya Mlandege FC ilishinda bao moja pekee na mtupiaji alikuwa ni Heritier Makambo.

Mchezo wa pili dhidi ya KMKM FC ilishinda mabao 2-1 hivyo inarejea Bongo ikiwa imeshinda mechi zote za kirafiki.

The post Yanga Warejea Bongo Kutoka Zanzibar appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz