Yanga: Simba Hawatupi Presha, Tunawapiga Tena-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Yanga: Simba Hawatupi Presha, Tunawapiga Tena-Michezoni leo

ZIKIWA zimesalia siku 13 tu kabla ya mchezo wa dabi ya Kariakoo ya mzunguko wa kwanza msimu huu, uongozi wa Yanga umeibuka na kuweka wazi kuwa hauna presha yoyote ya mchezo huo dhidi ya Simba, unaotarajiwa kupigwa Desemba 11, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa.

 

Yanga wanatarajiwa kuingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa dabi ya Kariakoo wa Ngao ya Jamii uliopigwa Septemba 25, mwaka huu kwenye Uwanja wa Benjamin MkapVinara hao wa msimamo wa Ligi Kuu Bara mpaka sasa wakiwa na pointi zao 16 walizokusanya kwenye michezo sita, leo Jumanne wanatarajiwa kuvaana na Mbeya Kwanza katika mchezo wa mzunguko wa saba wa Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema: “Kwetu jambo kubwa ni kuhakikisha tunaibuka na ushindi katika mchezo wetu wa Jumanne dhidi ya Mbeya Kwanza, hasa baada ya kupata matokeo ya sare kwenye mchezo dhidi ya Namungo.

 

“Kuhusiana na mchezo unaofuata dhidi ya Simba, sisi wala hatuna presha yoyote, tunaamini katika ubora wa kikosi tulichonacho na nikuhakikishie kuwa Desemba 11, kipigo chao kipo palepale.”

MAPYA KESI ya SABAYA, WASAIDIZI WAKE WALIDAI ni TISS, KAULI ya SAMIA Yazua GUMZO | FRONTPAGE

The post Yanga: Simba Hawatupi Presha, Tunawapiga Tena appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz