Yanga SC: Diarra Ataondoka Yanga-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Yanga SC: Diarra Ataondoka Yanga-Michezoni leo

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa hauna uhakika na mchezaji huyo kubaki ndani ya kikosi hicho kwa msimu ujao kutokana na uwezo alionao kwenye mikono yake na akili ya mpira.

 

Raia huyo wa Mali anaitwa Diarra Djigui huku jina la utani wakimuita ‘Screen Protector’ kutokana na kazi yake anayofanya akiwa kwenye lango.

 

Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara amesema kuwa kwa namna kijana huyo anavyofanya kazi kubwa akiwa uwanjani hana imani kama anaweza kubaki Yanga.

 

“Sijui kama Diarra atabaki Yanga kwa kuwa amekuwa kwenye ubora mkubwa, macho yake na masikio yake ni ya kimpira muda wote na mpaka basi zake pia ni za uhakika.

 

“Usajili wake wengi waliubeza lakini kwa sasa ninaona kwamba wengi wanaona kuna kitu ambacho kipo. Usajili wetu ulikuwa ni mzuri na umeleta wachezaji wazui na bora,” alisema Manara.

 

Kwenye ligi akiwa amecheza mechi tano Diarra amekusanya clean sheet nnne akifungwa bao moja na Shaban Msala wa Ruvu Shooting, Uwanja wa Mkapa.

 

LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam

 

The post Yanga SC: Diarra Ataondoka Yanga appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz