Wright: Jamani Solskjaer Kafika Mwisho Man Utd-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Wright: Jamani Solskjaer Kafika Mwisho Man Utd-Michezoni leo

STAA wa zamani wa Arsenal, Ian Wright, amesema kocha wa Man United, Ole Gunnar Solskjaer, hawezi
kubadilisha jambo lolote
kwenye timu hiyo kwa sasa na amefikia mwisho wa uwezo wake.

 

Kumekuwa na lawama nyingi kwa Solskjaer ndani ya Man United baada ya timu hiyo kushindwa kufanya vizuri kwenye michezo ya hivi karibuni, licha ya kujaza mastaa.“Nafikiri ameshafika mwisho, sioni kama anaweza kuisaidia tena Man United hapa ndiyo mwisho wake.

 

“Nafikiri kila mchambuzi kwa sasa amekuwa akizungumza jambo hilo, hakuna mwelekeo mpya, hakuna muunganiko na hakuna jambo lolote jipya pamoja na kwamba timu hiyo ina wachezaji mahiri.

 

“Nimewatazama wachezaji wa zamani wa Man United, Rio (Ferdinand), Roy Keane, naona nao wameanza kuzungumza jambo hilo,” alisema mshambuliaji huyo wa zamani.United ambao walikuwa wanapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu, baada ya michezo 11 wapo nyuma ya vinara Chelsea kwa pointi tisa.

The post Wright: Jamani Solskjaer Kafika Mwisho Man Utd appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz