Wachezaji Man United Wamkataa Ole Solskjaer-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Wachezaji Man United Wamkataa Ole Solskjaer-Michezoni leo

INAELEZWA kwamba Kocha wa Man United, Ole Gunnar Solskjaer anapata wakati mgumu kurejesha utulivu miongoni mwa wachezaji wa Man United huku ripoti zikidai kuwa wachezaji wakuu wana uhasama dhidi yake.

 

Haya yanajiri kufuatia matokeo duni ya United nyumbani ambayo imewashuhudia United wakijikokota kwenye nafasi ya sita jedwalini la msimamo wa Ligi Kuu Uingereza.

 

Mashetani Wekundu wamepoteza mechi sita kati ya 12 walizoshiriki huku kichapo cha hivi majuzi wakipokezwa na mahasidi wao wa jadi Man City wakati wa debi ya Manchester ugani Old Trafford. United walishindwa juzi na kupoteza 2-0 kwa City mnamo Jumamosi, Novemba 6 nyumbani.

 

Taarifa za ndani zinadai kwamba wachezaji wamemkataa kwa kuwa hana mbinu mbadala za ushindi badala ya kutegemea uwezo wa wachezaji, huku matumaini ya klabu hiyo waliokuwa nayo mwanzoni mwa msimu yakianza kuyeyuka.

 

Daily Mail inaripoti kuwa kocha huyo raia wa Norway anakumbana na ukinzani dhidi yake kutoka kwa wachezaji wakuu. Bruno Fernandes anaripotiwa kuongoza orodha ya wachezaji nyota wa Man United ambao wanahisi Solskjaer anapoteza klabu hiyo kwa kutotoa mwelekeo bora.

 

Kwa upande wake Cristiano Ronaldo, anahisi hadhi ya United imeshuka tangu aondoke klabuni humo miaka 12 iliyopita. Isitoshe, sehemu ya wachezaji wanasikitishwa na hali ya Donny van de Beek uwanjani Old Trafford.

 

Mholanzi huyo ameshushwa kimchezo tangu kuwasili kwake akitokea Ajax, huku Solskjaer akionekana kutokuwa na imani naye. Hatma ya Ole klabuni Man United Huku ikiaminika kuwa uongozi wa United wako tayari kusalia na kocha huyo hadi mwishoni mwa msimu, hatma yake inatakiwa kuamuliwa katika msimu huu.

 

Mshambulijai huyo mkongwe sasa anakumbanna hatma finyu klabuni hapo akipambana kurejesha imani yake na wafuasi. United wanatarajiwa kusafiri Vicarage Road kuvaana na Watford katika mechi yao nyingine ya EPL baada ya mapumziko ya kimataifa.

The post Wachezaji Man United Wamkataa Ole Solskjaer appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz