Tshishimbi Achekelea Kurudi Bongo-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Tshishimbi Achekelea Kurudi Bongo-Michezoni leo

NAHODHA wa zamani wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, amefunguka kuwa anafurahi kurudi Tanzania na kucheza soka kama ilivyokuwa awali.

 

Papy alisema Tanzania ni nchi ambayo aliishi kwa upendo, furaha na amani na amekuwa na marafiki wengi ambao alikutana nao akiwa anacheza Yanga.

Tshishimbi amerejea tena Tanzania na kusaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia timu ya Kitayose FC ya Tabora inayoshiriki Championship akiungana na nyota aliyepita Simba, Deo Kanda.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Papy alisema: “Nimefurahi kurudi tena Tanzania, sehemu ambayo niliishi vizuri na kupata marafiki wengi bado niko katika ubora, naahidi kuisaidia timu kufikia malengo ya kupanda daraja.

“Nimeshamalizana na hiyo timu, kazi yangu ni soka, siwezi kuchagua timu wala daraja la timu nitakayosajiliwa, naangalia maslahi kwanza.”

ISSA LIPONDA, Dar es Salaam

The post Tshishimbi Achekelea Kurudi Bongo appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz