TAIFA STARS YACHAPWA 3-0 NA DRC DAR-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

TAIFA STARS YACHAPWA 3-0 NA DRC DAR-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL Ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako nakutasoma habari zote hata kama hauna MB
MATUMAINI ya Tanzania kufuzu kwa mara ya kwanza Fainali za Kombe la Dunia yameanza kufifia baada ya kuchapwa mabao 3-0 nyumbani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Leopards yamefungwa na kiungo wa Lille ya Ufaransa, Gael Romeo Kakuta Mambenga dakika ya sita, beki wa Cape Town City ya Afrika Kusini, Nathan Idumba Fasika na mshambuliaji wa Sharjah ya Dubai, Ben Malango Ngita dakika ya 85.
Kwa matokeo hayo, Leopards inapanda kileleni mwa Kundi J ikiizidi pointi moja Taifa Stars kuelekea mechi za mwisho Jumapili.


Mechi nyingine ya Kundi hilo itachezwa Saa 1:00 usiku baina ya wenyeji, Benin wenye pointi saba pia na Madagascar yenye pointi tatu Uwanja wa l'Amitié Jijini Cotonou.
Kundi limezidi kuwa gumu kwa sababu sasa timu yoyote unaweza za kusonga mbele, kwani Madagascar wakishinda mechi mbili za mwisho watamaliza na pointi tisa na Taifa Stars inaweza kufuzu ikishinda mechi ya mwisho na endapo Benin na DRC zitatoa sare Jumapili Kinshasa.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz