Simba Haitaki Mazoea Kabisa Ligi Kuu-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Simba Haitaki Mazoea Kabisa Ligi Kuu-Michezoni leo

SIMBA haitaki mazoea! Unaweza kusema hivyo baada ya jana kuichapa kibishi Namungo bao1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Katika mchezo huo ambao ulishuhudiwa kiungo wa Namungo, Abdulaziz Makame akitolewa uwanjani kwa kadi nyekundu, bao la Simba lilifungwa na Meddie Kagere dakika chache kabla ya filimbi ya mwisho.

 

Huo ulikuwa ni mchezo wa tano kwa Simba msimu huu ndani ya Ligi Kuu Bara ambapo sasa imefikisha pointi 11 kutokana na kushinda mechi tatu na sare mbili. Bado haijapoteza.

Msimu uliopita baada ya mechi tano za kwanza, ilikuwa imekusanya pointi 13 baada ya kushinda mechi nne na sare moja.

 

Kabla ya mchezo wa jana, Simba ilianza msimu kwa suluhu dhidi ya Biashara United, kisha ikaifunga Dodoma Jiji 0-1 ugenini, ikarudi nyumbani kuifunga Polisi Tanzania 1-0, mchezo wa nne dhidi ya Coastal Union, ulimalizika kwa suluhu.

 

Hivi sasa kikosi hicho kipo chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Hitimana Thiery akisaidiana na Seleman Matola baada ya kuondoshwa kwa Kocha Mkuu, Didier Gomes.

 

Ushindi wa jana, umeifanya Simba kupanda hadi nafasi ya pili kutoka ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kufikisha pointi 11, ikiachwa pointi nne na vinara, Yanga wenye 15 ambao wameshinda mechi zote tano.Matokeo ya mechi zingine zilizochezwa jana Jumatano ni; Coastal Union 0-0 Prisons na Biashara United 0-0 Mbeya City

The post Simba Haitaki Mazoea Kabisa Ligi Kuu appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz