SAMATTA AIFUNGIA ANTWERP YATOA SARE UJERUMANI-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

SAMATTA AIFUNGIA ANTWERP YATOA SARE UJERUMANI-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL Ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako nakutasoma habari zote hata kama hauna MB


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana ameifungia bao la pili timu yake, Royal Antwerp ikitoa sare ya 2-2 ugenini dhidi ya wenyeji, Eintracht Frankfurt katika mchezo wa Kundi D UEFA Europa League Uwanja wa Deutsche Bank Park Jijini Frankfurt, Ujerumani.
Samatta alifunga dakika ya 88 baada ya kiungo Mbelgiji, Radja Nainggolan kufunga la kwanza dakika ya 33, wakati mabao ya Eintracht Frankfurt yalifungwa na Daichi Kamada dakika ya 12 na Gonçalo Paciência dakika ya 90.
Kwa sare hiyo, Antwerp inafikisha pointi mbili na kuendelea kushika mkia, wakati Eintracht Frankfurt inafikisha pointi 11 na kuendelea kuongoza kundi hilo, ikifuatiwa na Olympiakos ya Ugiriki yenye pointi tisa na Fenerbahce ya Uturuki yenye pointi tano.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz