Sakho, Mugalu Warejesha Furaha Simba-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Sakho, Mugalu Warejesha Furaha Simba-Michezoni leo

HABARI njema kwa mashabiki wa Simba ni kurejea kwa nyota wawili wa klabu hiyo, Pape Ousmane Sakho na
Chris Mugalu ambao tayari
wameanza mazoezi baada ya kukosekana kwenye michezo minne iliyopita kutokana na majeraha.


Mugalu na Sakho walipata
majeraha kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji uliopigwa Oktoba Mosi mwaka huu, ambapo kutokana na majeraha hayo mpaka sasa wamekosa michezo minne ya Simba katika mashindano yote.


Simba imeanza kwa
kusuasua msimu huu ambao mpaka sasa wanakamata nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi wakiwa wamejikusanyia pointi nane tu katika michezo minne waliyocheza mpaka sasa. Leo Simba wanatarajiwa kuikaribisha Namungo kwenye Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.


Akizungumza na Championi
Jumatano, Mkuu wa Maudhui wa Simba, Ally Shatry alisema: “Baada ya kuwa nje kwa muda mrefu kutokana na majeraha, tunatarajia wachezaji Sakho na Chris Mugalu watarejea kikosini baada ya kupona majeraha yao.

 

“Wachezaji hao wote wawili tayari wameanza programu za mazoezi, na kuendana na mahitaji ya benchi la ufundi tuna matumaini makubwa watakuja kuongeza nguvu katika michezo ijayo.”

Joel Thomas, Dar es Salaam

The post Sakho, Mugalu Warejesha Furaha Simba appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz