Saido, Makambo Waibua Vita Nzito Yanga SC-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Saido, Makambo Waibua Vita Nzito Yanga SC-Michezoni leo

UONGOZI wa Yanga baada ya kutangaza kuwa utamkosa mshambuliaji wake Yacouba Songne kwa zaidi ya miezi minne kutokana na majeraha aliyoyapata, mchezaji huyo ni kama ameacha vita ya namba kwa washambuliaji Saido Ntibazonkiza na Heritier Makambo kwa ajili ya kuchuana kuchukua nafasi ya mshambuliaji huyo.

 

Songne aliumia katika mchezo uliopita wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting ambapo katika mchezo huo, Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Uongozi wa Yanga tayari umethibitisha mchezaji huyo atapelekwa nchini Tunisia kwa matibabu akiambatana na daktari wa timu hiyo, Youssef Mohammed.

 

Katika mchezo uliopita wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting mara baada ya Yacouba kuumia, nafasi yake ilichukuliwa na Saido na akafanya vizuri.

 

Wakati huohuo pia kocha Nasreddine Nabi wa Yanga katika mchezo uliopita wa kirafiki dhidi ya Mlandege ya Zanzibar, alionekana akitumia mfumo wa washambuliaji wawili wa mbele ambao ni Fiston Mayele na Heritier Makambo jambo ambalo ni tafsri huenda akaamua kumrudisha Makambo ndani ya Yanga katika michezo ijayo ya ligi kuu baada ya Yacouba kukosekana.

 

Katika mchezo huo wa kirafiki Makambo alifanikiwa kuifungia Yanga bao pekee katika ushindi wa bao 1-0.

MARCO MZUMBE, Dar es Salaam

The post Saido, Makambo Waibua Vita Nzito Yanga SC appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz