Saido Amkuna Kocha wa Yanga Ligi Kuu-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Saido Amkuna Kocha wa Yanga Ligi Kuu-Michezoni leo

 

BAADA ya kiungo mshambuliaji wa Yanga, Said Ntibazonkiza ‘Saido’ kucheza mechi yake ya kwanza msimu huu ndani ya Ligi Kuu Bara, kocha mkuu wa timu hiyo, Nasreddine Nabi ameonekana kuvutiwa na uwezo wake.

 

Juzi Jumanne, Saido alicheza mechi dhidi ya Ruvu Shooting iliyochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar ambpo aliingia kipindi cha kwanza akitokea benchi kuchukua nafasi ya Yacouba Songne aliyeumia.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Kocha Nabi alisema: “Ntibazonkiza alicheza vizuri, ni mchezaji mkubwa na kila mtu anafahamu hilo, ndani ya Yanga kila mtu anayo nafasi ya kucheza kama ambavyo wengine hucheza.

 

Siwezi kusema kwa kuhakikisha atacheza katika michezo ijayo, lakini nafasi ni nzuri kwake kutokana na alichokionesha leo (juzi).”

STORI: MARCO MZUMBE, Dar es Salaam

The post Saido Amkuna Kocha wa Yanga Ligi Kuu appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz