Rasmi: Dean Smith Kocha Mpya Norwich City-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Rasmi: Dean Smith Kocha Mpya Norwich City-Michezoni leo

Klabu ya Norwich City imemteua Dean Smith kuwa kocha mpya wa kikosi hicho baada ya kumtimua Daniel Farke Novemba 7 mwaka huu. Smith amesaini kandarasi ya miaka miwili na nusu na atasaidia na Craig Shakespeare kama kocha msaidizi.

 

Smith ambae amefungashiwa virago kutoka Aston Villa, aliisaidia timu hiyo kupanda Ligi Kuu EPL, ndani ya msimu wake wa kwanza kabla ya kufuatiwa na misimu miwili ya mafanikio ndani ya EPL.

 

Smith kwa uzoefu wake vile vile aliisaidia Villa kufika Fainali ya kombe la Ligi msimu wa 2019/2020 lakini walipoteza mbele ya City katika uwanja wa Wembley.

 

Norwich kwa sasa inakamata nafasi ya mwisho katika msimamo wa EPL ikiwa na alama tano baada ya michezo 11. Je, Smith ataiepusha Norwich na janga la kushuka daraja mwishoni mwa msimu?

The post Rasmi: Dean Smith Kocha Mpya Norwich City appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz