Pacha wa Kagere Anukia Yanga-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Pacha wa Kagere Anukia Yanga-Michezoni leo

UNAMKUMBUKA mshambuliaji pacha wa Meddie Kagere kunako katika kikosi cha Gor Mahia ya Kenya, Jacques Tuyisenge,unaambiwa jamaa humuambii kitu kuhusu Ligi ya Tanzania huku akiweka wazi kuwa tayari kusajiliwa ndani ya Yanga kama itakuwa tayari kumchukua.

 

Tuyisenge na Kagere wamecheza wote ndani ya Gor Mahia, katika msimu wa mwaka 2017/18, kabla ya Kagere kuhamia Tanzania ambapo kwa sasa Tuyisenge anakipiga katika klabu ya APR ya Rwanda akiwa pia ndiye nahodha wa timu hiyo.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Tuyisenge alisema kuwa amekuwa akiifuatilia ligi ya Tanzania ambayo anatamani siku moja kuichezea kutokana na ubora wake kuzidi kukua huku akiweka wazi kuwa tayari kujiunga na Yanga kama itamuhitaji kama ambavyo iliwahi kutokea siku za nyuma.

 

“Ligi ya Tanzania ni ligi bora ambayo kwangu natamani kuona siku moja nacheza kwani naamini nitapata upinzani mzuri nikiwa katika ligi hiyo, kuna mashabiki wengi sana wanapenda mpira na mara nyingi wanajitokeza viwanjani ni jambo zuri sana.

 

“Kuhusu timu Yanga iliwahi kunihitaji lakini dili halikukamilika kutokana vitu ambavyo vilikuwa nje ya uwezo wangu lakini kama watakuwa na nia ya kunihitaji tena basi naamini itakuwa nafasi nzuri ya mimi kujiunga nao na kucheza katika ligi ya Tanzania,”alisema mshambuliaji huyo.

MARCO MZUMBE, Dar es Salaam

The post Pacha wa Kagere Anukia Yanga appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz