Pablo Awashtua Matola na Hitimana-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Pablo Awashtua Matola na Hitimana-Michezoni leo

UJIO wa Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco raia wa Hispania ambaye amepewa dili la miaka miwili umewashtua makocha waliokuwa kwenye timu hiyo kwa kuwa walikuwa hawafahamu lolote kuhusu kuwasili kwake Bongo.

Habari kutoka kwa mtu wa karibu wa makocha hao ilieleza kuwa Seleman Matola ambaye ni kocha msaidizi pamoja na Hitimana Thiery ambaye alikuwa ni Kaimu Kocha Mkuu wa Simba walikuwa hawajajui kuhusu Pablo.

“Makocha wameshtuka na ujio wa Pablo kwa kuwa hakuna ambaye alikuwa anajua kwamba anaweza kuja kwa ajili ya kupokea mikoba ya Didier Gomes hivyo ni kama imekuwa ni jambo la kushtukiza.

“Kikubwa ambacho walikuwa wanajua ni kwamba atakuja kocha atakuja ila kujua kwamba ni siku gani na anatokea nchi gani hapo ilikuwa ni shida kwao,” ilieleza taarifa hiyo.

Alipotafutwa Matola ili aweze kuzungumzia suala hilo alisema kuwa hawezi kuzungumza alipotafutwaMwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu hakuweza kupatikana.

LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam

The post Pablo Awashtua Matola na Hitimana appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz