Niyonzima Aingia Kwenye Vitabu vya FIFA-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Niyonzima Aingia Kwenye Vitabu vya FIFA-Michezoni leo

NAHODHA wa timu ya taifa ya Rwanda Haruna Niyonzima ameingia kwenye kumbukumbu za FIFA baada ya kuinga kwenye “FIFA’s Century Club” amabayo inawahusisha wachezaji waliocheza michezo 100 ya timu za taifa.

 

Mchezaji huyo wa klabu za As Kigali, Yanga na Simba alianza kuichezea timu yake ya taifa ya wakubwa mwaka 2006 na amefanikiwa kucheza michezo 104 na kufunga magoli 6 na kuwa mchezaji pekee aliyecheza michezo mingi kwenye timu ya taifa ya Rwanda.

 

Wachezaji ambao wanaingia kwenye FIFA’s Century Club ni wachezaji waliocheza michezo ya kombe la dunia, hatua ya mtoano, michezo ya kufuzu, kombe la mabara na fainali za Olimpiki kuanzia mwaka 1948 kwa waliocheza timu za wakubwa tu.

 

Mpaka tarehe 16 oktoba 2021 ni wachezaji 575 ambao wamefikisha michezo 100 ya huku kimataifa wakiwa na timu zao kulingana na nakala iliyotolewa na FIFA ya, Rec. Sport Soccer Statistics Foundation (RSSSF).

 

Katika jarida la RSSSF linamtambua Billy Wright kuwa ndie mchezaji wa kwanza kufikisha michezo 100 ya kimataifa akiwa na timu ya Uingereza mwaka 1959 akimaliza na michezo 105 wakati mchezaji aliyecheza michezo mingi ni s Bader Al-Mutawa wa kuwait akiwa na michezo 186.

The post Niyonzima Aingia Kwenye Vitabu vya FIFA appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz