Nabi Awakazia Mastaa Yanga-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Nabi Awakazia Mastaa Yanga-Michezoni leo

UNAAMBIWA kisa matokeo ya sare katika mchezo wao uliopita dhidi ya Namungo, kocha mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi ameonyesha kuwa hataki kuona wanadondosha pointi nyingine hii ni baada ya kuwakomalia mastaa wa timu hiyo katika maandalizi ya mchezo dhidi ya Mbeya Kwanza.

 

Yanga ambao ni vinara wa msimamo wa Ligi Kuu Bara mpaka sasa na pointi zao 16 walizokusanya kwenye michezo sita, Jumapili iliyopita kwa mara ya kwanza kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu walishindwa kuibuka na ushindi baada ya kupata sare ya bao 1-1 ugenini walipocheza dhidi ya Namungo.

 

Leo Jumanne Yanga watakuwa ugenini tena kuvaana na Mbeya Kwanza, mchezo unaotarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema: “Tulipata sare katika mchezo wetu uliopita dhidi ya Namungo ambayo ni wazi haikuwa mipango yetu, licha ya kwamba ni sehemu ya matokeo ya mchezo lakini kocha Nabi hakuridhishwa na mapungufu tuliyoyaonyesha.

 

“Tayari kocha amekaa na wachezaji na kuwasisitiza kuwa ni lazima tuhakikishe tunapambana kutodondosha pointi zaidi na kuibuka na ushindi katika mchezo wetu ujao dhidi ya Mbeya Kwanza.”

JOEL THOMAS, Dar es Salaam

The post Nabi Awakazia Mastaa Yanga appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz