Nabi Atua Taifa Kuwasoma Simba na Namungo-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Nabi Atua Taifa Kuwasoma Simba na Namungo-Michezoni leo

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nabi Nesreddine ni miongoni mwa watazamaji wa mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Namungo.

 

Kocha huyo ambaye ameiongoza Yanga kuibuka na ushindi kwenye mchezo mitano mfululizo ya Ligi Kuu Bara, anaonekana kuwa mtulivu huku akiwa ameshika tama ishara ya kuufuatilia mchezo huo kwa umakini mkubwa.

 

Nabi aliyevalia kofia nyeusi, anaonekana kuwasoma Namungo ambao baada ya wiki ya Kimataifa atakuwa na mchezo dhidi yao Novemba 20 huko kusini mwa Tanzania.

Hivyo hii ni fursa kwa Mtunisia huyo kuona namna gani mbavyo atawaandaa vijana wake kwa ajili ya mchezo huo. Ikumbukwe kuwa mara baada ya Yanga kucheza dhidi ya Namungo watarejea jijini Dar es Salaam kucheza dhidi ya Mbeya Kwanza kabla ya mchezo wa watani wa jadi, Desemba 11.

 

Nabi hayupo peke yake uwanjani hapa yupo na meneja wa Yanga, Hafidh Saleh licha ya kuwa wamekaa sehemu mbili tofauti mmoja, VIP A na mwingine B.

 

Mpaka mpaka mehi inafika mapumziko, sio Simba wala Namungo ambaye amefanikiwa kuona lango la mwenzake.

The post Nabi Atua Taifa Kuwasoma Simba na Namungo appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz