Nabi Anataka Rekodi ya Pasi Bongo-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Nabi Anataka Rekodi ya Pasi Bongo-Michezoni leo

KOCHA wa Yanga, Nasrredine Mohamed Nabi, amefunguka kuwa anahitaji timu yake iwe na uwezo mkubwa zaidi wa kumiliki mpira na kuwa na rekodi ya kupiga pasi nyingi kwenye kila mechi.

 

Nabi alisema soka la kisasa limebadilika sana kwa sababu timu yenye uwezo wa kumiliki mpira muda mrefu na kupiga pasi nyingi ndiyo huwa na nafasi ya kushinda mchezo kwa sababu wachezaji wanaongeza kujiamini.


Akizungumza na Global Publishers
, Nabi alisema timu yake imekuwa na uwiano mzuri kwenye kupiga pasi na kumiliki mpira, ila bado kuna kitu kidogo hakijakaa sawa na anakifanyia kazi baada ya muda mfupi timu hiyo itakuwa tishio zaidi kwenye pasi.


“Nahitaji timu
yangu na wachezaji wawe na uwezo wa kumiliki mpira zaidi ya sasa. Ubora wa kupiga pasi uwe juu zaidi na tuwe kati ya timu ambazo zina idadi kubwa ya pasi.


“Timu inayofanya hivyo
hujiweka kwenye mazingira mazuri ya kushinda mchezo. Kadiri unavyokaa na mpira muda mrefu timu inaongeza kujiamini na kumchanganya mpinzani, hicho ndiyo tunahitaji,” alisema Nabi.

The post Nabi Anataka Rekodi ya Pasi Bongo appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz