Mukoko Awekwa Sokoni Yanga SC-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mukoko Awekwa Sokoni Yanga SC-Michezoni leo

KIUNGO mkabaji Mkongomani wa Yanga, Mukoko Tonombe ni kati ya wachezaji huru katika kikosi hicho
wanaoruhusiwa kufanya
mazungumzo na klabu nyingine.


Huyo ni mchezaji wa pili katika
kikosi hicho cha Mtunisia, Nasreddine Nabi mwingine ni mshambuliaji Ditram Nchimbi ambaye amejitoa katika kikosi hicho.


Kiungo huyo hivi sasa
amekosa nafasi ya kudumu katika kikosi hicho tangu kuanza kwa msimu huu
ambao una viungo wengi bora
akiwemo Khalid Aucho na Yannick Bangala.


Akizungumza na Championi
Jumatatu, Mkurugenzi Uwekezaji na Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya timu hiyo, Injinia Hersi Said alisema Mukoko amebakisha miezi sita katika mkataba wake.


Said alisema kiungo huyo
alisaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu katika msimu uliopita na usajili wa dirisha dogo Januari ndiyo mkataba wake unamalizika.

 

Aliongeza kuwa aliyekuwa kiungo wao mshambuliaji, Tuisila Kisinda yeye alisaini mkataba wa miaka miwili kabla ya kumuuza kwenda klabu ya Berkane ya nchini Morocco.


“Kati ya kazi zenye ugumu ni
usajili wa wachezaji.“Kati ya wachezaji tuliopata nao ugumu basi ni akina Mukoko na Tuisila, kwani ili utoke na mchezaji nchini hapo lazima uwe na kibali maalum na ukikutwa naye Uwanja wa Ndege wa kwao na huna kibali, basi ujue una kesi.

 

“Usajili wa Mukoko ulikuwa wa mwaka mmoja na miezi ambao unamalizika Januari, mwaka huu na hivyo anaruhusiwa kufanya mazungumzo sasa na Kisinda yeye alisaini miaka miwili,” alisema Said.

STORI NA WILBERT MOLANDI NA MUSA MATEJA

#BREAKING: MILIPUKO MIWILI YAUA WATU UGANDA, HALI NI MBAYA, ASKARI WANAPAMBANA KUOKOA..

The post Mukoko Awekwa Sokoni Yanga SC appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz