Moloko Ajipa Kazi ya Kumng’arisha Mayele-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Moloko Ajipa Kazi ya Kumng’arisha Mayele-Michezoni leo

WINGA ya Yanga, Jesus Ducapel Moloko, amesema atahakikisha anaongeza juhudi katika kutengeneza nafasi kwa washambuliaji wao wakiongozwa na Fiston Mayele ili yapatikane mabao mengi.

 

Moloko amejiunga na Yanga msimu huu akitokea AS Vita ya DR Congo ambapo mpaka sasa ndani ya Ligi Kuu Bara amefanikiwa kufungia mabao mawili katika mechi tano, huku akiwa hana asisti.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Moloko aliweka wazi matanio yake ya kutengeneza nafasi nyingi za kufunga kwenda katika idara ya ushambuliaji huku akisema atahakikisha anaongeza juhudi kufanikisha hilo.

 

“Katika nafasi ambayo nacheza vitu vya msingi kwangu ni kutengeneza mabao pamoja na kufunga, tayari nimefanikiwa kutimiza moja lakini lingine bado sijafanikiwa.

 

“Natakiwa kutengeneza nafasi nyingi zaidi kwenda kwa washambuliaji ili waweze kufunga mabao ya kutosha, natamani kuona hilo nilikifanya.

 

“Bado kuna michezo mingi, nitapambana kuhakikisha safu ya ushambuliaji nawapikia mabao ya kutosha, nafahamu haitakuwa kazi nyepesi, lakini nitapambana kuhakikisha nafanikiwa,” alisema winga huyo raia wa DR Congo.

MARCO MZUMBE, DAR

The post Moloko Ajipa Kazi ya Kumng’arisha Mayele appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz