Mayele: Nitatumia Nafasi Zote Kufunga-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mayele: Nitatumia Nafasi Zote Kufunga-Michezoni leo

MARA baada ya kufanikiwa kufunga bao la ushindi katika mchezo wa kirafiki dhidi ya KMKM, mshambuliaji
wa Yanga, Fiston Mayele
amesema ataendelea kufunga kadiri atakapopata nafasi.


Katika mchezo huo uliochezwa
juzi Ijumaa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar, Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 yakifungwa na Jesus Moloko na Mayele. Awali iliifunga Mlandege 1-0 kupitia
Heritier Makambo.


Akizungumza na
Spoti Xtra, Mayele alisema: “Nafurahi kuona nimefunga bao muhimu na la ushindi kwa Yanga,
malengo yalikuwa ni
kushinda michezo yetu yote ya kirafiki, tumefanikiwa kwa hilo, tunawashukuru mashabiki
wote ambao wamejitokea
kutuunga mkono.


“Kuhusu kufunga mabao
natamani kuona kila siku nafunga, muhimu ni kutumia nafasi ambazo nitakuwa nazipata,
nitajitahidi natimiza hilo
kuhakikisha nafasi zote ambazo nitakuwa nazipata zinakuwa mabao.”

STORI: MARCO MZUMBE, DAR ES SALAAM

The post Mayele: Nitatumia Nafasi Zote Kufunga appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz