Mastaa Yanga Wala Kiapo Kuiua Mbeya Kwanza-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mastaa Yanga Wala Kiapo Kuiua Mbeya Kwanza-Michezoni leo

MASTAA wa Yanga ni kama wamekula kiapo kuhakikisha wanaibuka na ushindi dhidi ya Mbeya Kwanza leo Jumanne kutokana na kuweka wazi kuwa wanahitaji pointi tatu muhimu dhidi ya wapinzani wao kutoka Mbeya.

Yanga juzi Jumapili iliwasili tayari mkoani Mbeya kwaajili ya maandalizi ya mchezo huo unaotarajiwa kufanyika kesho katika Uwanja wa Sokoine jijini humo ambapo Mbeya Kwanza watakuwa wenyeji wa Yanga.

Kuelekea katika mchezo huo klabu ya Yanga ndiyo vinara wa ligi wakiwa wamejikusanyia jumla ya alama 16 mara baada ya kuibuka na ushindi katika michezo 5, huku mmoja wakitoka sare dhidi ya Namungo kwa bao 1-1.

Kiungo wa timu hiyo Feisal Salum alisema kuwa malengo yao wakiwa kama wachezaji ni kuhakikisha wanaibuka na ushindi mara baada ya kupata sare katika mchezo uliopita.

“Mchezo uliopita tulipata sare dhidi ya Namungo,tunashukuru ambacho tulikipata lakini kuelekea katika mchezo dhidi ya Mbeya Kwanza hakuna ambacho tunahitaji zaidi ya ushindi, tunafahamu tunakutana na timu ngumu lakini tutapambana kwa ajili ya ushindi.

Naye mshambuliaji Fiston Mayele kuelekea katika mchezo huo alisema kuwa :“Unajua kila ambaye tunacheza naye anatamani kuona anatafunga Yanga, sisi hatupo tayari kwa hilo na ndiyo maana tunatakiwa kuuona kila mchezo ambao upo mbele yetu kuwa ni fainali kwetu naamini kupitia hilo tutapata matokeo mazuri ambayo ni ushindi,”alisema mshambuliaji huyo.

The post Mastaa Yanga Wala Kiapo Kuiua Mbeya Kwanza appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz