Manara: Diarra Ana Side Mirror Yule – Video-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Manara: Diarra Ana Side Mirror Yule – Video-Michezoni leo

MSEMAJI wa klabu ya Yanga, Haji Manara amemsifu kocha wa timu hiyo, Nassredine Nabi kwa namna ambavyo timu hiyo inavyocheza soka lake la pasi nyingi.

 

Yanga katika mchezo wao uliopita dhidi ya Azam walipiga pasi 23 kuanzia kwa kipa mpaka wachezaji wa mbele na Jesus Moloko aliweka wavuni bao la pili.

 

Mtazame Msemaji wa Yanga SC, Haji Manara alipoamua kusimama wima akisifu uwezo wa golikipa wa timu hiyo Djigui Diarra

 

Manara amesema mpaka sasa katika timu yao wachezaji wao wote wanapiga pasi na hilo lilianza kujitokeza katika mchezo wao dhidi ya KMC.

 

“Tumepata ushindi wa mechi nne na haikuwa rahisi ilikuwa ni ushindi wa jasho na damu. Sisi sio tunapiga pasi tu kama wengine wanaopiga pasi wakiwa eneo lao, sisi tunapiga pasi na kwenda mbele.

 

“Kuna watu wanasema hata mwaka jana tuliongoza ligi baadae tukaachia, hatuwezi kuishi kwa kukariri kama mnakariri mbona hamkariri kuwa Yanga ni bingwa mara 27 karirini na hilo.

 

”Kuna dhambi naona inaanza kutengenezwa, wanaongelewa Aucho, Feisal na Bangala lakini husikii wakiongelewa Dickson Job wala Mwamnyeto ambao wamecheza dakika zaidi ya 400 na hawajaruhusu goli. Kwangu mimi Mwamnyeto sio mlinzi ni Holding Defender. Sisi tuna Timu, yule Diara ana side mirror, yaan anaona mbele kabla hata ya kupokea mpira.

 

“Mechi ya kesho vs Ruvu ina umuhimu mkubwa, tunakwenda kucheza kwa heshima ileile huku tukizasaka point tatu, Wana Yanga thamani yenu uwanjani ni kubwa zaidi ya mnavyofikiria.

 

“Tunacheza PPP yaani Piga pasi, Pokea na Pita mbele na hii imeanza kujitokeza katika mchezo wa Kmc lakini hata mchezo wa juzi bado tumeendelea,” amesema Manara.

 

Msemaji huyo mwenye mbwembwe nyingi amesema anamsifu kocha Nabi kwa kuitengeneza timu hiyo na sasa kucheza soka safi na la kuvutia.

 

“Nabi ni Profesa ameifanya Yanga kupiga pasi nyingi wakati huo huo timu ikipata ushindi, kumpongeza ni lazima kwa kazi anayoifanya,” amesema Manara.

The post Manara: Diarra Ana Side Mirror Yule – Video appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz