Lwanga, Mugalu Watibua Mipango ya Pablo-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Lwanga, Mugalu Watibua Mipango ya Pablo-Michezoni leo

KOCHA Mkuu wa Simba Muhispania, Franco Pablo anaumiza kichwa kwa kiungo wake mkabaji Mganda, Taddeo Lwanga na mshambuliaji Mkongomani, Chris Mugalu ambao huenda wakaukosa mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga.

 

Dabi hiyo inatarajiwa kupigwa Desemba 11, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam, mchezo unaotarajiwa kujaa upinzani mkubwa kwa Simba kulipa kisasi katika mchezo wa Ngao ya Jamii ambao walifungwa bao 1-0.

 

Wachezaji hao wapo nje ya uwanja kwa muda mrefu wakiuguza majeraha ya magoti wote wawili yaliyoyawasababishia kukosa michezo iliyopita ya Ligi Kuu Bara.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatatu, Pablo anatamani kuwatumia nyota hao kwa kuanzia mchezo huu wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Red Arrows uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Mkapa, lakini majeraha yamemvurugia.

 

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa wachezaji hao anafahamu umuhimu wao baada ya kupewa video za Lwanga na Mugalu za michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika ya msimu uliopita.

 

Aliongeza kuwa kukosekana kwa wachezaji wake hao kumevuruga mipango yake katika shirikisho na dabi ambayo amepanga kuanza kwa historia ya kuifunga Yanga katika ligi.

 

“Pablo alikuwa anatamani kuwatumia Lwanga na Mugalu lakini imeshindikana kutokana na wachezaji hao kupata majeraha.

“Wachezaji hao wote wapo katika mipango yake baada ya kuona uwezo wa kila mmoja kupitia video za michezo mbalimbali ikiwemo ya kimataifa na ligi.

 

“Mugalu yeye ameanza kupata nafuu kwa kuanza mazoezi mepesi ya binafsi, lakini Lwanga yeye bado kabisa yupo nyumbani kwao Uganda akiendelea na matibabu,”alisema mtoa taarifa huyo.

 

Alipotafutwa Kaimu Ofisa Habari wa timu hiyo, Ally Shatry kuzungumzia hilo alisema kuwa “Mugalu na Lwanga bado wana majeraha na watakosekana katika mchezo wa Red Arrows.

“Kwa upande wa Mugalu yeye ameanza kupata nafuu kwa kuanza mazoezi mepesi, lakini kwa Lwanga yeye bado hajaanza,”alisema Shatry.

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

The post Lwanga, Mugalu Watibua Mipango ya Pablo appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz