KOCHA WA REAL MADRID ATUA SIMBA SC -Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

KOCHA WA REAL MADRID ATUA SIMBA SC -Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL Ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako nakutasoma habari zote hata kama hauna MB


MABINGWA wa Tanzania, Simba SC wamemtambulisha Mspaniola, Pablo Franco Martín kuwa kocha wao mpya Mkuu anayechukua nafasi ya Mfaransa, Didier Gomes Da Rosa aliyefukuzwa mwishoni mwa mwezi uliopita.
Pablo aliyezaliwa Juni 11 mwaka ni kocha mwenye uzoefu aliyefundisha klabu mbalimbali nchini kwao, ikiwemo mabingwa wa kihistoria wa Ulaya, Real Madrid.
Pablo mwenye umri wa miaka 41, mzaliwa wa Madrid, alianza kufundisha Coria mwaka 2008 hadi 2009 akaenda Fuenlabrada kote kama Kocha Msaidizi.
Mwaka 2010 alikuwa Kocha Mkuu wa Santa Eugenia hadi 2012 Illescas akahamia Puertollano hadi 2014 akaenda Getafe B hadi 2015 Getafe A katika La Liga hadi 2016 akahamia Saburtalo Tbilisi ya Georgia hadi 2017.
Kutoka hapo akatua BSU ya China hadi akarejea Hispania na kuwa Kocha Maaidizi wa Real Madrid hadi 2019 alipojiunga na Al-Qadsia ya Kuwait hadi anahamia Simba SC mwezi huu.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz