Kocha Apigwa Risasi Katikati ya Mechi-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Kocha Apigwa Risasi Katikati ya Mechi-Michezoni leo

WACHEZAJI walilazimika kukimbia dimbani wakati mashabiki wa Klabu ya Hurucan Las Heras walipokuwa wakicheza dhidi ya Ferro de General Pico katika ligi ya kijimbo.

 

Kanda za video zilionesha wachezaji wa timu zote mbili wakikimbilia kujificha wakati risasi zilipofyatuliwa ndani ya uwanja huo uliopo mkoa wa Mendoza ambapo Kocha wa Ferro, Mauricio Romero alijeruhiwa na kukimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

 

”Romero kwa sasa anaendelea vyema na hayuko hatarini” , klabu ya Ferro ilisema katika taarifa yake katika mtandao wa twitter. Baada ya kuondoka uwanjani, alifanyiwa vipimo katika hospitali moja na baadaye kutoa taarifa kwa polisi.

 

Mechi hiyo ilisitishwa baadaye katika kipindi cha pili wakati walipokuwa wakiongoza 3-1 na Huracan imekosoa wale waliohusika katika tukio hilo. Mkufunzi mmoja wa kandanda alipigwa risasi katika bega wakati wa mechi ya daraja la tatu nchini Argentina siku ya Jumapili.

The post Kocha Apigwa Risasi Katikati ya Mechi appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz